Dalali ni nani?
Watu wengi katika kupata ardhi zao au nyumba za kupangisha wametumia watu wanaoitwa madalali. Tunafahamu kwa uchache juu ya shughuli zao wanazofanya kila siku.
Dalali ni mtu yeyote au taasisi inayofanya kazi ya uwakala ili kufanikisha biashara baina ya mteja na mtoa huduma fulani. Dalali ni mtu wa kati anayewaunganisha mteja na mwenye mali kwa kupata ujira unaotokana na kuwakutanisha pande mbili.
Nafasi ya Udalali
Ni kweli kwamba kwa sasa shughuli nyingi na biashara nyingi zinafanikishwa na uwepo wa madalali. Madalali wamekuwa kiungo kikubwa cha kufanikisha biashara na huduma mbali mbali sehemu za mjini na hata maeneo ya vijijini. Hali ya biashara ya kukutana mteja na mwenye mali imekuwa tofauti, matumizi ya madalali yamekuwa makubwa na yanaongezeka kila kukicha.
Katika sekta ya ardhi yaani ununuzi na ukodishaji wa nyumba, madalali wamekuwa kiungo muhimu katika kuwakutanisha wahitaji wa ardhi na nyumba pamoja na wamiliki na kufanikisha biashara au huduma.
Nisisitize kuwa kazi hii ya udalali ni nzuri pia ina tija kwenye jamii lakini wahusika wanapaswa kuifanya kwa kufuata misingi ya kazi ili jamii ikubali na kutofautisha kati ya udalali na utapeli.
Jisajili kaya.co.tz jaza fomu inayobainisha eneo unalafanyia shughuli muda mwingi wewe kama dalali pia kujitambulisha unachokifanya katika eneo hilo “About me”‘ mfano (Dalali wa nyumba, viwanja , mashamba , godown , yard, petrol stations fremu za biashara, vyumba, Maofisi nk. wasiliana nami. Karibu sana) utaonekana katika huu ukrasa kaya.co.tz/agents wanaohitaji nyumba na viwanja vya kununua au kupanga watakupata hapo.
Iko sawa
Asante, Karibu sana