Faida 5 za kuishi Pembezoni Majiji kama Dar es Salaam au Arusha.
Inapofikia wakati wa kufanya maamuzi ya sehemu ya kuishi, watu wengi wanapenda kuishi katikati ya jiji au karibu na jiji.
Sababu ni nini hasa?
- Ni nafuu.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa wa viwanja, nyumba za kupanga na kuuza bei zinakuwa kubwa sana katika majiji makubwa kama Dar es Salaam na Arusha. Na kadri unavyohitaji kupanga, kununua nyumba katikaki ya majiji au karibu sana na katikati ya jiji bei zinakuwa kubwa zaidi. Kwa kifupi, unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha pesa utapokuwa umefanya maamuzi ya kununua au kupanga pembezoni mwa jiji.
- Unapata eneo kubwa la kuishi.
Pamoja na kupata kitu kwa gharama nafuu, unapata kitu chenye thamani sawasawa na pesa unayolipa. Unamaweza kujikuta unapanga nyumba kubwa yenye bustani na parking kubwa sehemu ya nje ya jiji la Dar es Salaam kama vile Bunju, kwa nusu bei ya ile unayoweza kulipia nyumba ya ghorofani (apartment) ya vyumba viwili eneo la Mikocheni.
3.Unajinafasi zaidi
Kuishi sehemu ambayo wewe na jirani yako mnatenganishwa na ukuta kiasi kwamba unaweza hata kuyasikiliza mazungumzo yao kuna changamoto zake, ukiishi pambezoni mwa mji/jiji unaweza kupata sehemu ambayo wewe na jirani yako mnatenganishwa kwa mbali na inakuwa hakuna urahisi wa kuingiliana na jirani yako katika mambo mengi. Pia unaweza kujikuta unanunua na wewe sehemu yako kutokana na kuyazoea mazingira ya pembezoni mwa jiji na hii itategemea bajeti yako.
4. Unajenga msingi wa maisha yako ya baadaye.
Badala ya kutumia pesa nyingi katika kulipia kodi ya nyumba ili uweze kumudu kuishi karibu au katikati ya jiji, unaweza kuzitumia pesa hizo kununua kipande cha ardhi ambapo faida yake utaiona kwa maisha yajayo. Hata kama hutaweza kununua kipande cha ardhi, itakuwa raisi kwako kujiwekea akiba kutokana na fedha ambayo ungelipia kodi kubwa kama usingekuwa unaishi pembezoni mwa mji. Ukiachilia mbali yote, kutafuta mali au ardhi pembezoni mwa jiji kutakusaidia kujiwekea uwekezaji wa muda mrefu kwa faida yako na ya familia yako.
5. Tazama mbali sana unapohitaji nyumba ya kuishi.
Unapotafuta nyumba/apartment/upande/chumba cha kupanga fikiria kupata sehemu ambayo itakupatia furaha na amani. Sawa unaweza kufikiria kuwa ukiishi katika nyumba ambayo ipo karibu na eneo unalofanyia shughuli zako litakuwa jambo lenye tija. Lakini kumbuka pia wewe kuwa na furaha na amani ni kitu muhimu sana pengine kuliko kitu kingine chochote. Sawa, unaishi karibu na sehemu ya kazini kwako lakini unaishi sehemu yenye fujo nyingi zinazokuondolea furaha na amani. Kwa nini usitafute kuishi katika nyumba ambayo ukiishi unajisikia kuwa na amani na furaha? Nyumba ambayo ina eneo la kujinafasi, lina bustani za miti na maua na pengine hata mboga mboga ambazo hazina mbolea ya chumvi chumvi, sehumu ambayo unafuga hata kuku wa supu!