Kuishi Katika Nyumba Nzuri ni Haki Yako
Ishi katika Makazi bora yaliyopo katika maeneo yanayoloruhusu wakazi kufikia maeneo ya umma, fursa za ajira, huduma za afya, shule, vituo vya kulelea watoto na maeneo mingine muhimu ya kijamii
Usiishi mabondeni, maeneo ambayo husababisha majanga kwa wananchi wakati wa mvua, vikiwemo vifo na kuharibika kwa makazi yake.
Usiishi maeneo ambayo yanaathirika sana kwa mafuriko pale inaponyesha mvua kubwa
Usiishi katika mitaa ya mabanda na makazi yasiyo rasmi, kwenye nyumba zisizo bora au zisizokuwa na makazi kabisa.