Your search results

Majibu ya Maswali 8 Muhimu Zaidii Kuhusu kaya.co.tz

Posted by Admin Kaya on October 9, 2020
0


Kaya.co.tz ni mtandao unaowakutanisha wauzaji, wanunuzi, wapangaji na wapangishwaji wa Nyumba na Viwanja vinavyouauzwa au kupangishwa kutoka sehemu tofauti Tanzania.
Yafutayo ni baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa na watumiaji wa mtandao huu. Tumeweka majibu yake ili kuwasaidia watumiaji wetu kufahamu kaya.co.tz.


1.Ninawekaje tangazo langu kaya.co.tz
Ili kuweza kutangaza kuuza au kupangisha Nyumba au Kiwanja kaya.co.tz, inahitaji ufungue akaunti ya bure kabisa katika mtandao huu. Baada ya hapo, bofya kitufe kilichoandikwa (Post Ad/weka tangazo). Kisha ingiza taarifa za tangazo lako.
Ili tangazo lako liwe bora na zuri, hakikisha lina kichwa chenye jina la mali, maelezo rahisi na yanayoeleweka, bei na picha nzuri za mali. Tangazo lako litaonekana mtandaoni baada tu ya timu ya kaya.co.tz kulihakiki.

2. Utaratibu wa Kuhakiki Tangazo langu Unakuwaje?
Mara baada ya kuliweka tangazo lako lenye kiwango kinachokubalika, basi tangazo lako litaonekana kwa wepesi baada ya muhakiki kulipitia. Ili hii litokee vizuri inabidi kichwa cha tangazo kionekane vizuri, maelezo ya Tangazo lako yawe yanajitoshereze, na bei na picha ziwe sabia.
Lakini kama tangazo lako litakuwa lina tatizo , basi timu yetu ya wahakiki watakushauri nini cha kufanya ili kuliboresha na baada ya marekebisho tangazo lako litaonekana kwa wanunuzi. Tangazo lako litahakikiwa ndani ya masaa 48 kama utaliweka ndani ya masaa ya kawaida ya kazi. Kama ukiliweka ndani ya muda wa ziada wa kazi na siku za wikiendi, basi itachukua hadi masaa 7 kuhakikiwa. Baada ya tangazo kuruhusiwa, utapokea ujumbe kutoka kaya.co.tz kukutaarifu hili. Kama lilikataliwa, utapokea ujumbe wa barua pepe au kupigiwa simu kujulishwa nini tatizo. Hapo utaweza kulirekebisha na kuposti upya tangazo lako. Matangazo yako yote yatakuwa kwenye ubao wako wa matangazo ( dashboard).

3. Nawasiliana vipi na Muuzaji? kaya.co.tz ni mtandao unaowakutanisha wauzaji, wanunuzi, wapangaji na wapangishwaji wa nyumba na viwanja vinavyouzwa na kupangishwa. Lakini kaya.co.tz sio wauzaji wa nyumba na viwanja vinavyoonekana kwenye tovuti. . Ili kununua au kupanga nyumba au kiwanja unachokipenda , unaweza kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja kwa namna tofauti. Kama unatumia WhatsApp, bonyeza kwenye kitufe chenye nembo ya Whatsapp. Itafungua WhatsApp moja kwa moja ikiwa na namba ya muuzaji. Kama utataka kumpigia moja kwa moja, basi tumia kitufe kilichoandikwa call au unaweza kwenda sehemu iliyoandikwa ‘”Schedule a visit””na kujaza fomu iliyopo hapo.. Na pia unaweza kuwaitiana na Dalali kupitia barua pepe. Tumia sehemu ya barua pepe kama uko tayari kufanya hivyo

4. Ninaripoti vipi Udanganyifu wa Wauzaji au wapangishaji nyumba?
Pamoja ya kwamda kaya.co.tz ni mtandao wa kuaminika ikitokea Kama una mashaka ya aina yeyote na tangazo unaloliona wasiliana nasi tutapokea ripoti yako na kuchukua hatua mara moja. Tumia email moja kwa moja kwenda info@kaya.co.tz au kutupigie kupitia namba 0784225000 Tunawaomba wateja wetu wawiliane nasi kama wataona tatizo lolote.

5. kaya.co.tz Inasaidiaje Wauzaji, Wanunuzi, wapangaji na wapangishwaji wa Nyumba na Viwanja?
kaya.co.tz inatoa fedha muhimu juu ya biashara za kimitandao ili kuwasadia wauzaji wapate wateja wengi zaidi na wanunuzi,wapangaji kupata nyumba au viwanja i bora. Pia, kaya.co.tz inatoa elimu juu ya ulinzi wakati wa kufanya mauzo na manunuzi mitandaoni ili kuwalinda wateja wake. Haya yote yanatolewa kupitia blogu yake inayopatikana kupitia kaya.co.tz/blog.
6.Ninawasiliana Vipi na kaya.co.tz?
Kama ungependa kuwasiliana na kaya.co.tz kuna namna tofuati unazoweza kuzitumia kulingana na mahitaji yako. Unaweza kutupigia simu kupitia namba hii 0784225000. Pia unaweza kutuandikia barua pepe kupitia info@kaya.co.tz. Tuko kwenye mitandao ya kijamii ili kuwa karibu kabisa na wateja wetu. Huko unaweza kutu-follow kwa kutafuta kaya.co.tz kwenye mitandao ya kijamii na kutuuliza swali lolote. Na kama ukihitaji, unaweza kututembelea ofisini Upanga kwenye jengo la Amverton Office Park, barabara ya Magore na Lugalo. Tuko ghorofa ya pili.

  1. Nani anaweza kuweka Matangazo ya Nyumba na Viwanja kaya.co.tz? Dalali pekee ndio anaruhusiwa kuweka matangazo ya nyumba na viwanja katika kaya.co.tz.
    Hapa Dalali tuna maana ni mtu yeyote au taasisi inayofanya kazi ya uwakala ili kufanikisha biashara baina ya mteja na mtoa huduma fulani. Dalali ni mtu wa kati anayewaunganisha mteja na mwenye mali kwa kupata ujira unaotokana na kuwakutanisha pande mbili
    8.Kuna Gharama Zozote za Kuweka Tangazo kaya.co.tz?
    Hakuna gharama zozote za kuweka tangazo lako kwenye kaya.co.tz.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

  • Advanced Search

    TZS 4,000,000 to TZS 900,000,000

    TZS 30,000 to TZS 5,000,000

Compare Listings