Nyumba za Kupanga Sinza; Kwa nini ni chaguo la vijana wengi?
Eneo la Sinza, Dar es salaam ni maarufu sana na kwa miaka mingi vijana hupendelea kuishi huko. Mpaka kukapewa nickname ya ‘kwa wajanja’. Nyumba za Kupanga Sinza ni chaguo la vijana wengi wa rika la kati ambao hawaishi na familia (bachelors) au wenye familia ndogo ndogo.
Kuna sababu kuu TATU za vijana kupenda kupanga nyumba za Sinza ili kuishi na hata kufanya biashara. Sababu hizo ni kama ifuatavyo:-
- Urahisi wa Kodi
Urahisi wa kodi wa Nyumba za Kupanga Sinza umekuwa ni kivutio kwa vijana wengi wengi wenye kipato cha wastani. Hii ni kuanzia wale waliomaliza vyuo na kupata kazi zao za kwanza mpaka wale ambao ndio kwanza wanaanzisha familia. Ukilinganisha na maeneo mengine mengi ya jiji la Dar es salaam kama vile Mbezi beach, n.k gharama za maisha ya Sinza na standard yake ni rahisi kwa vijana wengi kuweza kuzimudu - Urahisi wa Usafiri
Kwa wakati wote wa mchana na usiku usafiri wa kwenda na kutoka Sinza kuelekea maeneo mbalimbali ya Dar es salaam upo na unapatikana kwa urahisi. Kwa mfano unahitaji basi moja tu kufika maeneo muhimu ya jiji kama vile soko kuu la Kariakoo, Kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo, Katikati ya jiji mjini Posta, Masaki, n.k. Hivyo basi Nyumba za Kupanga Sinza ni za thamani sana kwa vijana wenye kutaka kuelekea maeneo hayo maarufu kwa shughuli zao za kilasiku - Urahisi wa Upatikani wa Huduma Mbalimbali
Nyumba za kupanga Sinza zimezungukwa na sehemu za kutoa huduma mbalimbali zikiwemo maduka, migahawa, Nyumba za kulala wageni, hospitali na kadharika. Mfano migahawa na mabaa yako mengi na hayafungwi mapema, kwa mabachela na wanaofanya shughuli zao hadi usiku hufurahia sana maisha ya Sinza kwani wana uhakika wa kupata huduma muda wote.
Kuna maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam yenye nyumba zenye sifa mbali mbali ambazo zinaweza kuwa kivutio kwa vijana kuishi lakini nyumba za Sinza zimeendelea kuwa chaguo la vijana la muda wote kwa muunganiko wa sifa nyingi zaidi. Kwa mfano yapo maeneo ya jiji yenye kodi rahisi zaidi ya Sinza lakini vijana wengi hawapendezwi nayo kwa madai ya kiwango (standard) cha maisha ya sehemu hizo kwani kinaonekana kipo chini. Kwa maana kuna ugumu wa kufikika na kuna uhaba wa huduma mbalimbali mfano hospitali za uhakika na nyinginezo.
Kuna namna nyingi za kutafuta nyumba za kuishi katika eneo hili maarufu la Sinza ndani ya jiji la Dar es Salaam. Lakini njia iliyo rahisi na haraka kabisa ni ile ya kutembelea tovuti (website) ya www.kaya.co.tz ambayo itakupa nafasi ya kuona nyumba zinazopangishwa ama kuuzwa ndani ya Sinza na maeneo mengine mbalimbali ya majiji maarufu ndani ya Tanzania.