Your search results

USHAURI JINSI YA KUNUNUA VIWANJA

Posted by Admin Kaya on December 20, 2020
0

Na Emillian Rwejuna

Unapokosa ushauri mzuri wa jinsi ya kununua viwanja…matokeo yake unanunua kwa kutanguliza bajeti yako ndogo. Matokeo yake unanunua maeneo ambayo hayajapimwa, huduma za jamii hakuna. Hii ni sehemu mojawapo Dar es salaam ambapo usafiri pekee unaofika ni bodaboda….ili kufikisha barabara inabidi wananchi kuchangia gharama za kujenga barabara na pia huduma zingine kama umeme nk. Mwanzoni unafikiri umenunua kiwanja kwa gharama nafuu…kumbe utaendelea kulipia huduma za jamii kila siku kwa kipindi kirefu na mwishowe kujikuta unatumia hela nyingi kuliko aliyenunua kiwanja kwa bei ya juu….ila yeye haingii gharama za ziada kwa sababu huduma za jamii zinakuwa zimeishafika au ziko kwenye plan ya serikali kuzifikisha. Zingatia ushauri wa wataalamu ili kuepuka matatizo kama haya. Viwanja Tanzania tutakupatia ushauri bure na kukusaidia kuepuka matatizo kama haya. Karibu sana.

https://web.facebook.com/groups/2121341174631750

Leave a Reply

Your email address will not be published.

  • Advanced Search

    TZS 4,000,000 to TZS 900,000,000

    TZS 30,000 to TZS 5,000,000

Compare Listings