Waziri wa Ardhi, William Lukuvi afunga ofisi ya Ardhi na Masijala ya jiji la Dar es Salaam
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezifunga ofisi za ardhi na masijala za Jiji la Dar es Salaam.
Amechukua hatua hiyo leo Alhamisi Novemba 29, 2018 baada ya kubainika kuwa ofisi hizo ndio chimbuko la utapeli na ubadhilifu wa ardhi jijini humo.
Amesema jiji hilo halina ardhi, halipangi, halipimi na wala halimilikishi lakini bado hadi sasa wanaendelea kutoa ofa za ardhi ambazo zinaisumbua wizara yake, kubainisha kuwa shughuli zote za ardhi zitafanywa na wilaya tano za Dar es Salaam na kanda.
Amesema kwa sasa mtu yeyote mwenye ofa yenye muhuri wa jiji la Dar es Salaam hautatambulika na kuwataka wahusika kwenda katika manispaa kuuliza utaratibu mwingine.
Amesema wakishaingia kwenye mfumo wa kidigitali, ofisi za mikoa za ardhi hazitatambulika tena, kuanzia sasa maombi ya ardhi yatatoka wilayani kwenda kwa kamishna wa ardhi wa wilaya husika.
“Kuna watu wamekaa mkao wa kula kazi yao kuchapisha ofa za jiji, nilishatoa miaka miwili watu kwenye ofa hizi wazibadilishe kupitia kwa maofisa wa ardhi wa wilaya, kuanzia saa imekula kwao,” amesema Lukuvi.
“Tunatoa hati moja kwa moja hakuna ofa, nimeamua kufunga ofisi ya ardhi za jiji na watendaji wote wataripoti wizarani. Mawasiliano yatafanywa na manispaa yatakuja wizarani.”
Amesema kesho wafanyakazi wa ardhi katika ofisi hiyo iliyofungwa wanapaswa kuripoti kwa kamishna wa ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupangiwa kazi.
Chanzo: Mwananchi
For the English Audience
The Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, William Lukuvi, closes the Lands Department of the Dar es Salaam City Council.
He said Dar es Salaam City Council does not possess any land of its own and, as such, it has no mandate to offer or otherwise allocate land to anyone whatsoever.
In addition, he said that he had closed down the Council’s lands offices for issuing illegal land certificates, thereby “causing inconveniences and confusion at the Lands ministry.”
Thereafter, land applications should be submitted to the Commissioner for Lands in the respective administrative Districts.
The Minister also said that the Government would repossess all the plots of land that have remained undeveloped after they were allocated to people who applied for them under the government’s 20,000 Plots Project.’
He expressed disappointment that over 50% of the plot owners under the ‘20,000 Plots Project’ haven’t developed them, most being located at Bunju, Mpiji, Toangoma, Mwanagati, Kibada, Gezaulole, Mwongozo, Mbweni, Mbweni-Malindi, Mbweni-JKT and Kibada.
Apart from that he also directed the start of a house to house operation to identify house owners who have failed to collect from the ministry about 6,000 Certificates of Occupancy that were issued during the last 20 years and which are still lying on the ministry’s shelves